Aal-i-Imraan 3:37
آل عمرانفَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا ٱلْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَـٰمَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرْزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ
Basi Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipoingia chumbani kwake, alimkuta na vyakula. Basi alisema: Ewe Mariam! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hesabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu. [37]
[37] Mwenyezi Mungu alimpokea Maryamu kuwa ni nadhiri aliyo iweka mama yake, akamwitikia maombi yake, akamkuza makuzo mema, na akamlea katika kheri yake, Mola Mlezi, huku akimruzuku na kumshughulikia kwa malezi mazuri ya kumpa nguvu mwili wake na roho yake. Mwenyezi Mungu akamkabidhi Zakariya a.s. awe mlezi wake. Zakariya kila akiingia chumbani, alipo kuwa Maryamu anaabudu, akikuta chakula wasicho kizowea wakati ule. Zakariya akasema kwa kustaajabu: Ewe Maryamu! Umepata wapi riziki hii? Naye akamjibu: Hichi ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu. Ni shani yake kumruzuku mja wake amtakaye riziki nyingi bila ya hisabu au kipimo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Akamjibu maombi yake na Akaikubali nadhiri yake na kuipokea vizuri na Akamsimamia binti yake Maryam, kwa kumtunza na Akamkuza makuzi mazuri. Allah Mtukufu Akamsahilishia kwa kumjaalia Zakariyya, amani imshukie, kuwa ni mlezi wake; naye akamuweka mahali pake pa kuabudu. Na alikuwa kila akimjia mahali hapo, anakuta ana chakula kizuri kilichotayarishwa. Akasema, «Ewe Maryam, umepata kutoka wapi chakula hiki kizuri?» Akasema, «Hiyo ni riziki itokayo kwa Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu Anamruzuku Anayemtaka miongoni mwa waja Wake bila ya hesabu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net