Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 36

Aal-i-Imraan 3:36

آل عمران

فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّى وَضَعْتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّى سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّىٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ ٱلرَّجِيمِ

Maana

Basi alipomzaa, akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimemzaa wa kike - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa. Na wa kiume si sawa na wa kike. Na mimi kwa hakika nimemwita Mariam. Nami kwa hakika ninamkinga kwako, yeye na dhuria yake kutokana na Shetani aliyelaaniwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliye laaniwa. [36]

[36] Alipo jifungua mimba akasema kwa kujiudhuru kumwambia Mola wake Mlezi: Niliye mzaa ni mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua vilivyo alicho kizaa, na kuwa mwana wenyewe ni mwanamke ni bora kuliko alivyo taka mama kuwa awe mwanamume. Akasema yule mama: Mimi nimemwita Maryamu, na mimi nakuomba umlinde yeye na ukoo wake na uharibifu wa Shetani maluuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mimba yake ilipotimia na akamzaa mtoto wake alisema, «Mola wangu, mimi nimemzaa mwanamke ambaye hafai kwa kutumikia Baitulmaqdis,» Na Allah Mtukufu Anajua zaidi kwa alichokizaa na atamjaalia kuwa na jambo kubwa. Mke wa ‛Imrãn aliendelea kusema, «Na Mwanamume niliyemtaka kwa kutumika si kama Mwanamke kwa hilo. Kwa kuwa mwanamume ni mwenye nguvu zaidi wa kutumika na kusimamia utumishi. Na mimi nimempa jina la Maryam. Na mimi nimemlinda kwako, yeye na watoto wake, kutokana na Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema Yako».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net