Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 35

Aal-i-Imraan 3:35

آل عمران

إِذْ قَالَتِ ٱمْرَأَتُ عِمْرَٰنَ رَبِّ إِنِّى نَذَرْتُ لَكَ مَا فِى بَطْنِى مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّىٓ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Aliposema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimekuwekea nadhiri kilicho katika tumbo langu la uzazi awe mtumishi wako, basi nikubalie. Hakika, Wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [35]

[35] Ewe Nabii! Taja hali ya mke wa Imran alipo weka nadhiri wakati alipo kuwa na mimba, kuwa mwana aliomo tumboni mwake awe ni wa kumtumikia Mwenyezi Mungu tu na kukhudumia nyumba yake. Alisema: Ewe Mola! Hakika mimi nimekuwekea nadhiri huyu aliyomo tumboni mwangu awe ni wa kukhudumia nyumba yako, basi nikubalie haya. Hakika Wewe ni Mwenye kusikia kila kauli, na Mwenye kujua kila hali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Mtume, ilivyokuwa kuhusu mambo ya Maryam na mama yake na mtoto wake ‛Ĩsã, amani imshukie, ili kuwarudi, kwa hayo, wale wanaodai uungu wa ‛Ĩsã au kuwa yeye ni Mwana wa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, aliposema mke wa ‛Imrãn wakati aliposhika mimba, «Ewe Mola wangu, mimi nimekutakasia kilioko ndani ya tumbo langu kiwe ni chako Peke Yako kwa kutumikia Baitulmaqdis. Basi takabali kutoka kwangu. Hakika Wewe Peke Yako Ndiye Msikizi wa dua yangu, Ndiye Mjuzi wa nia yangu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net