Aal-i-Imraan 3:34
آل عمرانذُرِّيَّةًۢ بَعْضُهَا مِنۢ بَعْضٍ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Ni dhuria wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [34]
[34] Amewakhitari hao ukoo ulio safi, wakirithiana usafi na fadhila na kheri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maneno ya waja wake kwa vitendo vyao na vinavyo fichwa vifuani mwao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Manabii hawa na Mitume ni mlolongo wa usafi wenye kuungana katika kumtakasa Allah Mtukufuna, kumpwekesha na kutenda vitendo vinavyoambatana na wahyi Wake. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, ni Mjuzi wa vitendo vyao na Atawalipa kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net