Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 33

Aal-i-Imraan 3:33

آل عمران

إِنَّ ٱللَّهَ ٱصْطَفَىٰٓ ءَادَمَ وَنُوحًا وَءَالَ إِبْرَٰهِيمَ وَءَالَ عِمْرَٰنَ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Hakika, Mwenyezi Mungu alimteua Adam, na Nuhu, na ukoo wa Ibrahim, na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote. [33]

[33] Kama Mwenyezi Mungu alivyo mteua Muhammad afikishe ujumbe wake, na akajaalia kumfuata Muhammad ni njia ya kufikia mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kupata maghfira na rehema yake, kadhaalika ametaja Mwenyezi Mungu kuwa Yeye alimteua Adam na akamjaalia ni katika wateule wa walimwengu. Pia alimteua Nuhu kwa kumpa ujumbe, na akamteua Ibrahim na ukoo wake, nao ni Ismail na Is-haq na Manabii wengine kutokana na wana wao hao. Miongoni mwao ni Musa a.s. Akawakhitari ukoo wa Imran, na miongoni mwao akamkhitari Isa na mama yake. Alimfanya Isa awe ni Mtume kwa Wana wa Israili, na Maryam akamfanya awe ni mama wa Isa bila ya baba.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Amemchagua Ãdam, Nûḥ, jamii ya Ibrãhîm na jamii ya ‛Imrãn Akawafanya kuwa ni bora wa watu wa zama zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net