Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 32

Aal-i-Imraan 3:32

آل عمران

قُلْ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Sema: 'Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume.' Na wakigeuka, basi hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri. [32]

[32] Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakikukataa basi hao ni makafiri, wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, Mtiini Allah Mtukufu kwa kufuata Kitabu Chake, na mtiini Mtume kwa kufuata mwenendo wake wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake.Wakiwa watakupa mgongo na kukomaa kwenye ukafiri na upotevu walionao, wao hawatakuwa wanastahili mapenzi ya Allah Mtukufu. Kwani Allah Mtukufu Hawapendi makafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net