Aal-i-Imraan 3:31
آل عمرانقُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِى يُحْبِبْكُمُ ٱللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atawapenda na atawafutia dhambi zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. [31]
[31] Sema: Ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu, kuwa mnampenda Mwenyezi Mungu na mnataka Mwenyezi Mungu akupendeni, basi nifuateni mimi kwa ninayo kuamrisheni na ninayo kukatazeni. Kwani mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu atakupendeni kwa hivyo, na atakulipeni kwa kukufanyieni hisani na kusamehe makosa yenu. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kuwasamehe na kuwarehemu waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Ikiwa nyinyi munampenda Allah Mtukufu kikweli, nifuateni mimi na kuniaminini, ndani na nje, ndipo Allah Mtukufu Atawapenda na Atawasamehe madhambi yenu.Kwani Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya waja Wake Waumini, ni Mwingi wa rehema kwao.» Aya hii tukufu yamhukumu kila anayedai kumpenda Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na akawa hamfuati Nabii Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kama ipasavyo kufuatwa, na wala hamtii katika maamrisho yake na makatazo yake, kuwa yeye ni mrongo katika madai yake mpaka amfuate Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kama ipasavyo kufuatwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net