Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 30

Aal-i-Imraan 3:30

آل عمران

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوٓءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُۥٓ أَمَدًۢا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفْسَهُۥ ۗ وَٱللَّهُ رَءُوفٌۢ بِٱلْعِبَادِ

Maana

Siku ambayo kila nafsi itakuta yale iliyofanya katika mema yamehudhurishwa, na pia yale iliyofanya katika ubaya. Itapenda lau baina ya hayo (mabaya) na yeye ungekuwepo umbali mrefu. Na Mwenyezi Mungu anawatahadharisha na yeye mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyo yafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilio ufanya. Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. [30]

[30] Basi na watahadhari wale wanao ikhalifu amri yake na Siku ambayo kila mtu atakuta vitendo vyake vya kheri hata kilicho kichache kimeletwa hadharani; na pia uovu wake alio utenda ambao angetamani lau kuwa uko mbali, mwisho wa umbali, hata asiuone kwa kuuchukia na kukhofu kutumbukia katika adhabu zake. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni na adhabu zake pindi mkitokana na ulinzi wake na utawala wake, ambao ni upole na rehema kwa waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na katika Siku ya Kiyama, Siku ya Malipo, kila nafsi italikuta jema lolote ililolifanya linaingojea likiwa limeongezwa ili ilipwe nalo. Na pia baya iliolifanya italikuta linaingojea vilevile, hapo itatamani lau ingekuwa baina yake na hilo tendo baya zama zirefu. Basi jitayarisheni kwa Siku hii, na muogope mateso ya Mola Aliye Jabari. Na pamoja na ukali wa mateso Yake, Yeye, Aliyetakasika na sifa za upungufu, ni Msifika kwa ukamilifu wa huruma kwa waja.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net