Aal-i-Imraan 3:29
آل عمرانقُلْ إِن تُخْفُوا۟ مَا فِى صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ ٱللَّهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Sema: Mkificha yaliyo vifuani mwenu au mkiyaweka wazi, Mwenyezi Mungu anayajua. Na anayajua yaliyo katika mbingu na yaliyo katika dunia. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyafichua Mwenyezi Mungu anayajua; na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [29]
[29] Sema, ewe Nabii!: Mkiyaficha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha katika vitendo vyenu na kauli zenu ni sawa, kwani Mwenyezi Mungu anayajua yote, na anayajua yote yaliymo mbinguni na yaliyomo duniani, yanayo onekana na yanayo fichikana. Uwezo wake unapenya katika viumbe vyake vyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, Kuwaambia Waumini, Mkiyaficha yaliyomo ndani ya nyoyo zenu ya kuwafanya makafiri ni wategemewa na wasaidizi au mkiyadhihirisha hayo, hakitafichika chochote katika hayo kwa Allah Mtukufu. Kwani ujuzi Wake umezunguka kila kilichoko mbinguni na kilichoko ardhini, na Ana uwezo kamili juu ya kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net