Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 28

Aal-i-Imraan 3:28

آل عمران

لَّا يَتَّخِذِ ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ ٱللَّهِ فِى شَىْءٍ إِلَّآ أَن تَتَّقُوا۟ مِنْهُمْ تُقَىٰةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفْسَهُۥ ۗ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa marafiki wa kuwasaidia badala ya Waumini. Na mwenye kufanya hilo, basi hatakuwa na chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anawahadharisha naye mwenyewe. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. [28]

[28] Ikiwa basi ni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ndiye Yeye peke yake Mmiliki wa mamlaka, anatukuza na kuangusha, na katika mikono yake pekee ipo kheri, na uumbaji, na riziki, basi haifai kwa Waumini kuwafanya wasio kuwa Waumini wawe na utawala juu yao, wakauwacha msaada wa Waumini wenzao. Kwani wakifanya haya inakuwa wanaivunja Dini, na wanawaletea maudhi wenye Dini, na ni kuudhoofisha utawala na udugu wa Kiislamu. Na mwenye kufuata njia hii basi kwa Mwenyezi Mungu Mmiliki wa mamlaka yote hana lake jambo. Wala haimfalii Muumini kuridhia kuwapa utawala na ulinzi makafiri ila awe hana hila. Hapo basi anaweza kujikinga na madhara yao kwa kuonyesha ut'iifu kwao. Ni juu ya Waumini wawe daima katika ulinzi wa Kiislamu, kwani huo ndio ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Na watahadhari wasitoke kwenye ulinzi wa Mwenyezi Mungu kuuendea ulinzi mwenginewe asije akawaadhibu kwa kuwaletea madhila baada ya utukufu. Na kwake Yeye ndio marejeo, wala hapana pa kukimbilia kutokana na madaraka yake duniani wala Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anawakataza Waumini kuwafanya makafiri kuwa ni wategemewa, kwa mapenzi na kwa kutaka himaya, badala ya Waumini. Na yoyote mwenye kuwafanya wao ni wategemewa, huyo ameshakuwa mbali na Allah Mtukufu, na Allah Mtukufu Yuko mbali na yeye. Isipokuwa mkiwa ni madhaifu wenye kuogopa, hapo Allah Mtukufu Amewapa ruhusa muwasairi ili kujiepusha na shari lao, mpaka mtakapopata nguvu. Na Allah Mtukufu Anawatahadharisha nyinyi na Yeye. basi mcheni na muogopeni. Na Kwake Peke Yake ndio marejeo ya viumbe kwa kuhesabiwa na kulipwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net