Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 27

Aal-i-Imraan 3:27

آل عمران

تُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ ٱلْمَيِّتَ مِنَ ٱلْحَىِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ

Maana

Wewe huuingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hesabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wewe huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hisabu. [27]

[27] Na Wewe kwa ulivyo umba na ukawekea sababu na nyendo, unauingiza usiku katika mchana kwa unavyo zidi mchana urefu wake, na unauingiza mchana katika usiku kwa unavyo zidi usiku urefu wake. Na unatoa chenye sifa za kuonekana kihai katika kisicho kuwa na sifa za uhai, kama unavyo toa chenye kukosa uhai kutokana na kilicho hai, chenye kutamakani na sababu za uhai. Unampa neema zako kubwa umtakaye kwa mujibu wa mipango ya hikima zako. Hapana mchunguzi wa kukuhisabu Wewe. Huyo Mwenye shani hii haemewi na kumjaalia Mtume wake na awapendao, ubwana, na utawala, na utajiri, na wasaa, kama alivyo waahidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa dalili za uwezo Wako, ni kuwa Wewe Unautia usiku ndani ya mchana, na Unautia mchana ndani ya usiku, huu ukarefuka na ule ukafupika. Na Unatoa chenye uhai kutoka kwa kilichokufa kisichokuwa na uhai, kama kutoa mazao kutokana na mbegu na kama kumtoa Muumini kutoka kwa kafiri. Na Unatoa kilichokufa kutoka kwa chenye uhai, kama kutoa yai kwenye kuku. Na Unamruzuku Unayemtaka katika waja Wako bila hesabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net