Aal-i-Imraan 3:26
آل عمرانقُلِ ٱللَّهُمَّ مَـٰلِكَ ٱلْمُلْكِ تُؤْتِى ٱلْمُلْكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلْمُلْكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُ ۖ بِيَدِكَ ٱلْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye Mmiliki wa ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye. Na humtukuza umtakaye, na humdhalilisha umtakaye. Heri yote iko mkononi mwako. Hakika, Wewe ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu. [26]
[26] Ewe Nabii! Sema kwa unyenyekevu na kuukiri utukufu wake Mwenyezi Mungu: Ewe Mola Mlezi! Ni Wewe peke yako ndiye Mwenye kumiliki kutasarafu katika mambo yote. Unampa kuhukumu na utawala umtakaye, na unamnyima umtakaye. Unampa utukufu umpendaye kati ya waja wako kwa kumwezesha kuzishika sababu za kuufikia huo utukufu. Na unampiga madhila na unyonge umtakaye. Basi Wewe peke yako unamiliki kheri yote. Hushindwi na kitu katika kutimiza muradi wako na yanayo kupelekea hikima yako kuyakatia shauri katika mipango ya uumbaji wako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema ,ewe Nabii, ukielekea kwa Mola wako kwa dua, «Ewe Ambaye Una ufalme wote, Wewe Ndiye Ambaye Unamtunuku ufalme, mali na umakinifu katika ardhi Umtakaye miongoni mwa waja Wako, na Unauondoa ufalme kutoka kwa Umtakaye. Na Unampa enzi ya ulimwengu na ya Akhera Unayemtaka, na Unamfanya awe na unyonge Unayemtaka. Kheri ipo mikononi mwako. Wewe, Peke Yako, juu ya kila kitu, ni Muweza.» Katika ayah hii pana kuthibitisha sifa ya Mkono kwa Allah Mtukufu kwa namna inayonasibiana na Yeye, utakatifu ni Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net