Aal-i-Imraan 3:25
آل عمرانفَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَـٰهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Basi itakuwaje tutakapowakusanya kwa ajili ya Siku ambayo hakuna shaka nayo? Na kila nafsi italipwa ilichochuma, nao hawatadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi itakuwaje tutakapo wakusanya Siku ambayo haina shaka kuja kwake? Na kila nafsi italipwa kama ilivyo chuma, bila ya kudhulumiwa. [25]
[25] Basi itakuwaje hali yao wakati atapo wakusanya Mwenyezi Mungu Siku ya Akhera, ambayo hapana shaka kuwapo kwake, na kuwa kutakuwapo kuhisabiwa. Basi kila nafsi itapewa malipo yake ya kutosha. Na wao wanastahili kupata hiyo adhabu ya Jahannamu watakayo ipata.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Vipi hali zao zitakuwa, Atakapowakusanya Allah Mtukufu ili wahesabiwe katika Siku isiyo na shaka kuja kwake, nayo ni Siku ya Kiyama, na kila mmoja apate malipo ya aliyoyatenda, na wao bila kudhulumiwa kitu chochote?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net