Aal-i-Imraan 3:24
آل عمرانذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا۟ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامًا مَّعْدُودَٰتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِى دِينِهِم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Hayo ni kwa sababu walisema: "Hautatugusa Moto isipokuwa kwa siku chache tu." Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe walikuwa wakiyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo kuwa wakiyazua. [24]
[24] Hao wanao kataa miongoni mwa Mayahudi wamedanganyika kwa kukataa kwao na matumaini ya uwongo wanao jitamanisha nafsi zao ya kuwa Moto hautawagusa ila siku chache tu. Na kudanganyika huko na matamanio hayo yamewapelekea kuendelea kuzua katika dini yao kunako endelea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
kujiepusha huko na haki, sababu yake ni itikadi mbaya walionayo Watu wa Kitabu kwamba wao hawataadhibiwa isipokuwa siku chache. Itikadi hii iliwapelekea wao wamfanyiye ujasiri Allah Mtukufu na waidharau Dini Yake na waendelee na dini yao ya batili ambayo walijidanganya nayo nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net