Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 23

Aal-i-Imraan 3:23

آل عمران

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَـٰبِ ٱللَّهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ

Maana

Je, huwaoni wale waliopewa fungu katika Kitabu? Wanaitwa kukiendea Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kihukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao wanageuka huku wamepeana mgongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaitwa kukiendea Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao; kisha baadhi yao wanageuka wanakikataa. [23]

[23] Je! Huijui hali ya wale walio pewa sehemu ya Kitabu na ilimu (nao ni Mayahudi na Wakristo) wanaitwa wende kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho ni Qur'ani ili kiwapambanulie baina ya Kweli na uwongo, Haki na baat'ili, katika khitilafu zilizo zuka baina yao, na wala hawafanyi haraka ya kumuitikia anaye waita. Bali baadhi yao wanamkataa; shani yao ni kuukataa wito wa kheri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, umeona, ewe Mtume, hali ya kustaajabisha zaidi kuliko hali ya hawa Mayahudi, ambao Allah Mtukufu Amewapa fungu katika Kitabu wakajua kuwa yale uliyoyaleta ni haki, wanaitwa wafuate yaliyokuja katika Kitabu cha Allah Mtukufu, nacho ni Qur’ani, ili kitoe uamuzi katika mambo waliotafautiana juu yake, kisha wengi wao wanakataa uamuzi huo iwapo haulingani na matamanio yao, kwa kuwa desturi yao ni kuipa mgongo haki?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net