Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 22

Aal-i-Imraan 3:22

آل عمران

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ

Maana

Hao ndio ambao vitendo vyao viliharibika duniani na Akhera. Nao hawana wowote wa kuwanusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika duniani na Akhera. Nao hawatapata wa kuwanusuru. [22]

[22] Watu wenye sifa kama hizo, a'mali zao zimebat'ilika ijapo kuwa baadhi yake ni njema, na hazina matunda. Kwa hivyo haziwafai duniani, na mwisho wake ni hizaya na adhabu huko Akhera. Na wala hawana wa kuwaokoa na khasara na adhabu watayo ipata.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao amali zao zilichanguka ulimwenguni na Akhera. Hakuna amali yao yoyote itakubaliwa, na hawatakuwa na yoyote mwenye kuwanusuru kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net