Aal-i-Imraan 3:21
آل عمرانإِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَيَقْتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ ٱلَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِٱلْقِسْطِ مِنَ ٱلنَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Hakika, wale wanaozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawaua Manabii bila ya haki, na wakawaua wale wanaoamrisha haki katika watu, basi wabashirie adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali. [21]
[21] Hakika wale wanao zipinga Ishara za Mwenyezi Mungu katika uumbaji na hizi zilizo teremka, na wakawauwa Manabii alio watuma Mwenyezi Mungu waje kuwaongoa - bila ya haki kabisa, na hiyo ni dhulma kubwa mno - na wakawauwa wale wanao waita watu wafanye haki na uadilifu, watu hao wanastahiki adhabu kali. Basi wabashirie adhabu hiyo!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale wanaozikanusha dalili zilizo wazi na yale waliokuja nayo Mitume, wakawaua Manabii kwa udhalimu bila haki yoyote, na wakawaua wale ambao wanaamrisha uadilifu na kufuata njia ya Mitume, wape bishara ya adhabu yenye uchungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net