Aal-i-Imraan 3:20
آل عمرانفَإِنْ حَآجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِىَ لِلَّهِ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْأُمِّيِّـۧنَ ءَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا۟ فَقَدِ ٱهْتَدَوا۟ ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ ٱلْبَلَـٰغُ ۗ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِٱلْعِبَادِ
Na wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na vile vile walionifuata. Na waambie wale waliopewa Kitabu na wale wasiojua kusoma: "Je, mmesilimu?" Wakisilimu, basi hakika wameongoka. Na wakikengeuka, basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona vyema waja wake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basi wameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake. [20]
[20] Na hawa makafiri wakijadiliana nawe katika Dini hii baada ya wewe kuwapa hoja zote, huna haja kupigizana nao kelele kwa majadiliano. Waambie tu: Mimi na Waumini walio nifuata tumemsafia Mwenyezi Mungu peke yake ibada yetu. Na waambie Mayahudi na Wakristo na washirikina wa Kiarabu: Dalili zimekwisha bainika kwenu, basi silimuni. Wakisilimu inakuwa wameijua njia ya uwongofu na wameifuata. Na wakikataa huna lawama wewe kwa kukataa kwao. Waajibu wako ni kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu tu. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema waja wake. Hapana lolote lao, hali yao na vitendo vyao, linalo fichikana kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakijadiliana na wewe, ewe Mtume, Watu wa Kitabu juu ya Tawhîd: kumuwahidisha na kumpwekesha Allah Mtukufu, baada ya kuwasimamishia hoja, waambie, «Mimi nimemtakasia Allah Mtukufu Peke Yake, si mshirikishi Yeye na yoyote; na pia wale Waumini walionifuata wamemtakasia Allah Mtukufu na kumtii.» Na waambie wao na wale washirikina, Waarabu na wengineo, «Mkiingia kwenye Uislamu, basi nyinyi muko kwenye njia ya sawa, uongofu na haki. Na mkirudi nyuma, hesabu yenu iko kwa Allah Mtukufu. Mimi sina langu isipokuwa ni kufikisha ujumbe. Na mimi nimewafikishia na nimesimamisha hoja juu yenu.» Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaona waja, hakuna chochote chenye kufichika kwake katika mambo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net