Aal-i-Imraan 3:19
آل عمرانإِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلْإِسْلَـٰمُ ۗ وَمَا ٱخْتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ
Hakika, Dini kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na hawakuhitilafiana wale waliopewa Kitabu isipokuwa baada ya kujiwa na elimu, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na mwenye kuzikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. [19]
[19] Hakika Dini ya Haki aliyo iridhi Mwenyezi Mungu ni Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja, na kumnyenyekea Yeye kwa usafi wa moyo. Mayahudi na Wakristo wamekhitalifiana na Dini hii, wakazua na wakabadilisha. Na wala kukhalifu kwao hakukuwa kwa kudanganyikiwa au kwa ujinga ilipo wajia ilimu, bali yalikuwa hayo kwa uhasidi na ushindani tu. Na mwenye kupinga Ishara za Mwenyezi Mungu, basi na angojee hisabu ya Mwenyezi Mungu, nayo yenda kasi mno.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika dini ambayo Allah Mtukufu Aliwachagulia waja Wake na Akawatumiliza kwayo Mitume Wake na ambayo Hakubali isipokuwa hiyo ni Uislamu. Nao ni kumnyenyekea Allah Mtukufu, Peke Yake, kwa kumtii na kujisalimisha Kwake kwa udhalilifu na kuwafuata Mitume katika yale waliotumilizwa kwayo katika kila kipindi mpaka wakahitimishwa kwa kuja Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ambaye, Hakubali Allah Mtukufu dini kutoka kwa yoyote, baada ya kutumilizwa kwake, isipokuwa Uislamu ambao alitumilizwa nao. Na tafauti baina ya Watu wa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, iliyowafanya watengane wawe mapote na makundi, haikutokea ila baada ya kuthibiti hoja juu yao kwa kupelekwa Mitume na kuteremshwa Vitabu; hiyo ilitokana na uadui na uhasidi kwa kutafuta ulimwengu.Na yoyote mwenye kuzikanusha aya za Allah Mtukufu zilizoteremshwa na alama Zake zenye kujulisha umola Wake na uungu Wake, basi Allah Mtukufu ni Mwepesi wa hesabu, na Atawalipa kwa yale waliokuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net