Aal-i-Imraan 3:18
آل عمرانشَهِدَ ٱللَّهُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَأُو۟لُوا۟ ٱلْعِلْمِ قَآئِمًۢا بِٱلْقِسْطِ ۚ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Mwenyezi Mungu alishuhudia kuwa hakika hakuna mungu isipokuwa Yeye, na pia (walishuhudia) Malaika, na wenye elimu akisimamisha uadilifu. Hakuna mungu isipokuwa Yeye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [18]
[18] Mwenyezi Mungu amebainisha wazi katika maumbaji yake dalili na Ishara ambazo hawezi kuzipinga mwenye akili, ya kwamba Yeye ni Mmoja, wala hana mshirika wake, na kwamba Yeye ndiye Mwenye kusimamia mambo ya viumbe vyote kwa uadilifu. Na kwa haya pia wamekiri Malaika walio t'ahirika, na wameyajua watu wa ilimu kwa yakini, na kwamba Yeye ilio tukuka shani yake ni Mpweke katika Ungu, wala hana wa kumshinda katika jambo, na hikima yake imeenea kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Ameshuhudia kuwa Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa uungu. Na Ameambatanisha ushahidi wake na ule wa Malaika na watu wa elimu juu ya kitu kitukufu zaidi chenye kushuhudiwa, nacho ni Tawhîd umoja Wake Aliyetukuka na kusimamia Kwake haki na uadilifu. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliye Mshindi Ambaye hakuna kitu Atakacho kiwe kikakataa kuwa, Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net