Aal-i-Imraan 3:17
آل عمرانٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلْقَـٰنِتِينَ وَٱلْمُنفِقِينَ وَٱلْمُسْتَغْفِرِينَ بِٱلْأَسْحَارِ
Wanaovumilia, na wakweli, na wanyenyekevu, na watoao, na wanao omba msamaha katika masaa ya mwisho ya usiku.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanao subiri, wanao sema kweli, na wat'iifu, na wanao toa sadaka, na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri. [17]
[17] Na malipo haya huyapata wanao stahamili mashaka kwa ajili ya ut'iifu wao, na kujitenga na maasi, na kuvumilia dhiki, watu ambao ni wakweli katika kauli zao na vitendo vyao, na niya zao, wenye kudumu katika ut'iifu kwa kunyenyekea, wenye kutoa wawezacho bilhali walmali na vyenginevyo kwa sababu ya mambo ya kheri, ambao kwamba wanamtaka msamaha Mwenyezi Mungu mwishoni mwa usiku, kabla ya alfajiri, zinapo safika roho na hutengenea kuzingatia na kutafakari katika utukufu wa Muumbaji.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa ndio waliosifika kwa subira juu ya kumtii Allah Mtukufu, kuepuka maasia na juu ya shida zinazowafikia zilizokadiriwa na Allah Mtukufu. Na ndio waliosifika kwa ukweli wa maneno na vitendo na kutii kikamilifu. Na ndio waliosifika kwa utoaji, wa siri na wadhahiri na kwa kuleta istighfãr: kuomba msamaha, katika mwisho wa usiku, kwa kuwa wakati huo unatarajiwa zaidi kukubaliwa amali na kujibiwa dua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net