Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 16

Aal-i-Imraan 3:16

آل عمران

ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ إِنَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Maana

Wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumeamini. Basi tusamehe dhambi zetu, na tuepushe kutokana na adhabu ya Moto.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto, [16]

[16] Malipo haya watayapata wale ambao nyoyo zao zimejaa Imani, na wakatangaza kwa ndimi zao wakisema kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu: Mola Mlezi wetu! Hakika sisi tumeamini kwa kuitikia wito wako. Basi tusamehe dhambi zetu, na utuhifadhi na adhabu ya Moto.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waja hawa wacha Mungu huwa wakisema, «Mola wetu, sisi tumekuamini Wewe na tumemfuata Mtume Wako Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, tusamehe madhambi tuliyoyatenda na utuepushe na adhabu ya Moto».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net