Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 15

Aal-i-Imraan 3:15

آل عمران

قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَٰجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِٱلْعِبَادِ

Maana

Sema: Je, niwaambie yaliyo bora kuliko hayo? Kwa waliomcha Mungu kwa Mola wao Mlezi ziko Bustani zipitazo mito chini yake. Watadumu humo, na wake waliotakaswa, na radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona vyema waja wake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Nikwambieni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wachamngu ziko Bustani kwa Mola wao zipitazo mito kati yake. Watadumu humo, na wake walio takaswa, na wanazo radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake. [15]

[15] Ewe Nabii! Sema: Nikwambieni yaliyo bora kuliko hayo yote mliyo pambiwa duniani? Kwa wale wachamngu wamewekewa malipo ya dhamana kwa Mola wao Mlezi, nayo ni Bustani zipitazo mito chini ya vivuli vya miti. Humo watastarehe kwa maisha mazuri wala hawatoingiliwa na khofu ya kuwa neema hiyo itaondoka, kwani wamekwisha katibiwa kuwa humo watabaki daima milele. Watakuwamo humo wake walio t'ahirika, wamesafika na kila ila ya wanawake wa kidunia. Na juu ya yote hayo, watapata Radhi ya Mwenyezi Mungu ambayo wataihisi chini ya kivuli chake kuwa ndiyo Neema kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali za waja wake; hapana jambo linalo fichikana kwake, hawana siri asiyo ijua Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema ,ewe Mtume, «Je, ni wape habari ya yaliyo bora kuliko yale waliyopambiwa watu katika maisha haya ya kilimwengu? Wale waliomcha Allah Mtukufu na wakaogopa mateso Yake, watakuwa na Pepo ambazo inapita mito chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Watakaa milele humo. Na watakuwa nao humo wake waliotakasika na hedhi na nifasi na tabia mbaya. Na watakuwa na malipo makubwa zaidi kuliko hayo, nayo ni radhi za Allah Mtukufu.» Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuona siri za viumbe wake, ni Mjuzi wa hali zao na atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net