Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 14

Aal-i-Imraan 3:14

آل عمران

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلْبَنِينَ وَٱلْقَنَـٰطِيرِ ٱلْمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلْفِضَّةِ وَٱلْخَيْلِ ٱلْمُسَوَّمَةِ وَٱلْأَنْعَـٰمِ وَٱلْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسْنُ ٱلْمَـَٔابِ

Maana

Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundo mingi ya dhahabu na fedha, na farasi wazuri zaidi, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani, na Mwenyezi Mungu ana marejeo mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema. [14]

[14] Wanaadamu wameumbwa kuwa wanapenda matamanio ya vitu kama wanawake, wana, na wingi wa madhahabu na fedha, na farasi wazuri wazuri walio fundishika, na mifugo kama ngamia, ng'ombe, mbuzi, kondoo, na kadhaalika mashamba makubwa. Lakini yote hayo ni starehe na kwa matumizi ya uhai huu wa duniani wenye kupita na kuondoka. Na hayo si chochote si lolote ukilinganisha na hisani anayo wafanyia Mwenyezi Mungu waja wake wanao pigania jihadi katika Njia yake watakapo rejea kwake Yeye Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wamepambiwa watu kupenda matamanio ya wanawake na watoto wa kiume na mali mengi ya dhahabu, fedha, farasi wazuri, wanyama wa mifugo miongoni mwa ngamia, ng’ombe na mbuzi na kondoo na ardhi inayotayarishwa kwa kupandwa miti na wakulima. Hayo ni mazuri ya uhai wa kilimwengu na pambo lake lenye kutoweka. Na kwa Allah Mtukufu kuna marejeo mazuri na thawabu, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net