Aal-i-Imraan 3:13
آل عمرانقَدْ كَانَ لَكُمْ ءَايَةٌ فِى فِئَتَيْنِ ٱلْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَـٰتِلُ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْىَ ٱلْعَيْنِ ۚ وَٱللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِۦ مَن يَشَآءُ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُو۟لِى ٱلْأَبْصَـٰرِ
Hakika, mlikuwa na Ishara katika yale makundi mawili yalipokutana (katika vita). Kundi moja likipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, nalo lingine kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho. Na Mwenyezi Mungu humuunga mkono amtakaye kwa nusura yake. Hakika, katika hayo kuna mazingatio kwa wenye macho yaliyo sawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika ilikuwa ni Ishara kwenu katika yale majeshi mawili yalipo pambana. Jeshi moja likipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jingine kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho. Na Mwenyezi Mungu humuunga mkono amtakaye kwa nusura yake. Hakika katika hayo yapo mazingatio kwa wenye macho. [13]
[13] Ilikuwa Ishara wazi na mazingatio yaliyo dhaahiri katika makundi mawili ya wapiganaji walipo pambana siku ya Badri. Kundi moja, hilo la Waumini, likipigana kwa ajili ya kutukuza Neno la Mwenyezi Mungu na kueneza Haki. Na kundi la pili, hilo la makafiri, likipigania pumbao na matamanio. Ikawa, basi, Mwenyezi Mungu katika kuwaunga mkono Waumini aliwafanya wale makafiri wawaone Waumini idadi yao mara mbili kuliko walivyo. Kwa hivyo makafiri wakaingiwa na khofu nyoyoni mwao wakaemewa. Na Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Katika haya, hakika, pana mazingatio kwa wenye nadhari iliyo ongoka isiyo kengeuka na kuiacha Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika yalikuwa kwenu, enyi Mayahudi wakaidi, ni ushuhuda mkubwa yale mapambano ya Badr yaliyotokea baina ya makundi mawili: kundi moja linapigana kwa ajili ya Dini ya Allah Mtukufu, nalo ni kundi la Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na Masahaba wake, na kundi lingine lenye kumkanusha Allah Mtukufu, linapigana kwa ajili ya batili. likiwatazama Waumini kwa macho linawaona kuwa ni mara mbili ya ile idadi yao. Na Allah Mtukufu Alilifanya hilo kuwa ni sababu ya ushindi wa Waislamu juu yao. Na Allah Mtukufu Anawasaidia kwa nusura Yake anaowataka katika waja Wake. Hakika katika tukio hili pana mazingatio makubwa kwa wenye busara ambao wanaongokea kujua hukumu zake na matendo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net