Aal-i-Imraan 3:12
آل عمرانقُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
Waambie wale waliokufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa mtiwe kwenye Jahannam; napo ndipo pahali paovu zaidi pa mapumziko.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waambie walio kufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa, mtiwe kwenye Jahannam; nako huko ni makao mabaya kabisa. [12]
[12] Ewe Nabii! Waambie hawa walio kufuru: Bila ya shaka nyinyi mtashindwa hapa duniani, na kesho Akhera mtaadhibiwa. Na Jahannamu ndio itakuwa tandiko lenu la kulalia; na ovu lilioje tandiko hilo!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia makafiri miongoni mwa Mayahudi na wengineo na wale ambao waliudharau ushindi wako katika Badr, «Nyinyi mtashindwa duniani na mtakufa ukafirini, na mtakusanywa mpelekwe kwenye Moto wa Jahanamu, ambao utakuwa ni tandiko la milele kwenu; tandiko baya sana ni hilo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net