Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 11

Aal-i-Imraan 3:11

آل عمران

كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Maana

Kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao. Walikadhibisha Ishara zetu, basi Mwenyezi Mungu akawachukua kwa dhambi zao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama yaliyo wapata watu wa Firauni na wale walio kuwa kabla yao. Walikanusha Ishara zetu, basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa madhambi yao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. [11]

[11] Na hali ya hao ni kama hali ya kaumu ya Firauni walio kuwa na inda kabla yao. Walizikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu juu ya kuwa zilikuwa ziwazi kabisa. Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa sababu ya madhambi waliyo yatenda. Na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali ya makafiri katika kukanusha kwao na adhabu itakayowashukia ni kama hali ya jamaa za Fir’aun na wale makafiri waliokuwa kabla yao. Wao walizikanusha aya za Allah Mtukufu zilizo wazi, Allah Mtukufu akawapatiliza kwa kuwatesa kwa sababu ya kukanusha kwao na kushindana. Na Allah Mtukufu ni Mkali wa kutesa kwa aliyemkufuru Yeye na kuwakanusha Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net