Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 10

Aal-i-Imraan 3:10

آل عمران

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَن تُغْنِىَ عَنْهُمْ أَمْوَٰلُهُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمْ وَقُودُ ٱلنَّارِ

Maana

Kwa hakika, wale waliokufuru, hazitawafaa kitu mali zao wala watoto wao kutokana na Mwenyezi Mungu. Na hao ndio kuni za Moto.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wale walio kufuru hazitowafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu mali zao, wala watoto wao; nao hao ndio kuni za Motoni. [10]

[10] Katika Siku hiyo makafiri hawatokingwa na mali yao na yangawa mengi vipi, wala na watoto wao na wangawa wengi vipi. Hayo yote yatakuwa ndio kuni za Moto za kuwateketeza wenyewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliokanusha Dini ya haki na wakaikataa, hayatawafaa wao mali yao wala watoto wao kuwaepushia chochote katika adhabu ya Allah Mtukufu ikiwashukia ulimwenguni, wala hayatawakinga wao na adhabu Yake Akhera. Na hawa ndio kuni za Moto Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net