Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 41

Aal-i-Imraan 3:41

آل عمران

قَالَ رَبِّ ٱجْعَل لِّىٓ ءَايَةً ۖ قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَـٰثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗ وَٱذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِبْكَـٰرِ

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipokuwa kwa kuashiria tu. Na mtaje Mola wako Mlezi kwa wingi, na mtakase jioni na asubuhi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipo kuwa kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Mola Mlezi wako kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi. [41]

[41] Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi amfanyie alama ya kuhakikisha bishara hii. Mwenyezi Mungu akamjibu: Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu muda wa siku tatu, isipo kuwa utatumia ishara tu kuashiria utakacho. Na shikamana na dhikri ya Mwenyezi Mungu ukimtakasa na kumtukuza jioni na asubuhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Zakariyyã akasema, «Mola wangu, nijaalie alama ambayo itakuwa ni dalili kwangu ya kupata matoto ili nipate kuingiwa na furaha na bashasha.» Akasema, Alama yako uliyoitaka ni kutoweza kusema na watu kwa siku tatu isipokuwa kwa Kuwaashiria, pamoja na kuwa wewe uko sawa na mzima. Na katika kipindi hiki, kithirisha Kumtaja Mola wako na umswaliye katika nyakati za mwisho wa mchana na mwanzo wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net