Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 194

Aal-i-Imraan 3:194

آل عمران

رَبَّنَا وَءَاتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ

Maana

Mola wetu Mlezi! Na tupe yale uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika, Wewe huvunji miadi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi. [194]

[194] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Tupe uliyo tuahidi kwa ndimi za Mitume yako, nayo ni ushindi na kuungwa mkono duniani. Wala usituingize Motoni ukatuhizi Siku ya Kiyama. Shani yako ni kuwa huendi kinyume na miadi yako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Mola wetu! Tupe yale uliyotuahidi kwenye ndimi za Mitume wako, ya kupata ushindi, umakinifu, taufiki na uongofu. Wala usitufedheheshe, kwa madhambi yetu, Siku ya Kiyama. Hakika wewe ni Mkarimu, Huendi kinyume na ahadi ulizowaahidi waja wako.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net