Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 193

Aal-i-Imraan 3:193

آل عمران

رَّبَّنَآ إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِى لِلْإِيمَـٰنِ أَنْ ءَامِنُوا۟ بِرَبِّكُمْ فَـَٔامَنَّا ۚ رَبَّنَا فَٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّـَٔاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ ٱلْأَبْرَارِ

Maana

Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumemsikia mwitaji akiita kwenye Imani kwamba: 'Muaminini Mola wenu Mlezi'; kwa hivyo, tukaamini. Basi tufutie dhambi zetu, na utufunikie makosa yetu, na utufishe pamoja na walio wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema. [193]

[193] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika sisi tumemsikia Mtume wako akiita watu wakuamini Wewe, nasi tukamt'ii na tukamuamini. Ewe Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu makubwa, na tufutie maovu yetu madogo madogo, na baada ya kufa kwetu tujaalie tuwe pamoja na waja wako walio bora.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Mola wetu! Sisi Tumemsikia mlinganizi, naye ni Mtume wako Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, anawaita watu wakuamini Wewe na kukubali Umoja wako na kuzifuata kivitendo Sheria zako, tukauitikia ulinganizi wake na tukauamini utume wake. Basi tusamehe madhambi yetu, uzisitiri aibu zetu na utukutanishe na watu wema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net