Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 192

Aal-i-Imraan 3:192

آل عمران

رَبَّنَآ إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ ٱلنَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُۥ ۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

Maana

Mola wetu Mlezi! Hakika, yule unayemwingiza Motoni, basi umemhizi. Na waliodhulumu hawana wasaidizi wowote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio dhulumu hawana wasaidizi. [192]

[192] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika mwenye kustahiki Moto na ukamuingiza, basi umempa hizaya. Na mwenye kudhulumu akastahiki Moto hana wa kumnusuru nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Mola wetu! Tuokue na Moto, kwani hakika Wewe, ewe Allah Mtukufu, yoyote Utakayemuingiza Motoni kwa madhambi yake, ushamfedhehesha na kumdhalilisha. Na watenda madhambi, wanaozidhulumu nafsi zao, hawatakuwa na yoyote wa kuwatetea wasipate adhabu ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net