Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 188

Aal-i-Imraan 3:188

آل عمران

لَا تَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَآ أَتَوا۟ وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا۟ بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا۟ فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ ٱلْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Kamwe usiwadhanie wale wanaofurahia yale waliyoyafanya, na wakapenda kwamba wasifiwe kwa yale ambayo hawakuyatenda. Basi kamwe usiwadhanie kuwa watasalimika kutokana na adhabu. Na wana adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Usiwadhanie kabisa wale wanao furahia waliyo yafanya, na wakapenda kusifiwa kwa wasiyo yatenda, usiwadhanie kuwa watasalimika na adhabu. Yao wao ni adhabu chungu. [188]

[188] Usiwadhanie kabisa kuwa wataepuka adhabu wale wanao tenda maovu, na wakapenda kusifiwa kwa wasilo lifanya. Shani yao hao ni kujifungia mlango wa Imani na Haki, kama Mayahudi. Nao watapata adhabu chungu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwadhanie wale wanaofurahia matendo maovu waliyoyafanya, kama Mayahudi, wanafiki na wengineo, na wakawa wanapenda kuwa watu wawataje vizuri kwa mambo ambayo hawakuyafanya, basi msiwadhanie wao kuwa ni wenye kuokoka na adhabu ya Allah Mtukufu duniani. Na watakuwa na adhabu iumizayo kesho Akhera. Katika haya kuna onyo kali kwa kila mwenye kutenda kitendo kiovu na kukifurahia na kwa kila mwenye kujigamba kwa ambacho hakukifanya ili watu wamsifu na kumshukuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net