Aal-i-Imraan 3:187
آل عمرانوَإِذْ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَـٰقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ لَتُبَيِّنُنَّهُۥ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُۥ فَنَبَذُوهُ وَرَآءَ ظُهُورِهِمْ وَٱشْتَرَوْا۟ بِهِۦ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ
Na pale Mwenyezi Mungu alipochukua agano la wale waliopewa Kitabu kuwa: 'Bila shaka mtawabainishia watu, na wala hamtakificha.' Lakini wakakitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani ndogo. Basi ni kiovu mno hicho wanachokinunua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho nunua. [187]
[187] Ewe Nabii! Kumbuka na utaje pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi madhbuti kwa Watu wa Kitabu, kuwa wayaeleze wazi maana ya Kitabu chao, na wala wasiwafiche watu chochote, na wao wakakitupilia mbali nyuma ya migongo yao, na badala yake wakatafuta starehe za dunia. Na starehe za dunia kama zitakavyo kuwa ni kitu chenye thamani duni kabisa kulinganisha na uwongofu na uwongozi. Ama wamejua kutenda uovu! (Hayo yalikuwa zamani na bado yanaendelea. Kuficha na kugeuza na kupotosha Biblia hakusiti. Vipo vitabu vyao vinavyo itwa "Apokrifa", maana yake "Vilivyo fichwa", kwa kuwa hivyo ni marfuku visisomwe ila na mapadri tu, na vingine vimeteketezwa. Miongoni mwa hivyo ni Injili ya Barnaba.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Allah Mtukufu Alipochukua ahadi ya mkazo juu ya wale ambao Allah Mtukufu Amewapa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, Mayahudi walipewa Taurati na Wanaswara walipewa Injili, ili wavitumie na wawafahamishe watu yaliyomo ndani yake wala wasiyafiche. Lakini wao waliiacha ahadi hiyo na hawakujilazimisha nayo. Na wakachukua thamani duni ikiwa ni badali ya wao kuificha haki na kukipotoa Kitabu. Ni mabaya yalioje manunuzi waliyonunua ya kuipoteza kwao ahadi na kubadilisha kwao Kitabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net