Aal-i-Imraan 3:186
آل عمرانلَتُبْلَوُنَّ فِىٓ أَمْوَٰلِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوٓا۟ أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ ٱلْأُمُورِ
Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu, na nafsi zenu. Na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na wale walioshirikisha. Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu, basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutokana na walio pewa Kitabu kabla yenu na wale walio shiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamchamungu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia. [186]
[186] Kuweni na yakini, enyi Waumini, kuwa mtapata mitihani na majaribio katika mali yenu, kwa kupungua, kutoa au kunyang'anywa, na katika nafsi zenu kwa Jihadi au kuuwawa au kwa maradhi na machungu. Na kadhaalika mtasikia kutokana na Mayahudi na Wakristo na mapagani, washirikina, matusi na uchokozi wa kukuudhini. Na mkiyakaabili hayo kwa kuvumilia na kumcha Mwenyezi Mungu basi itakuwa ni katika mambo mema yanayo wajibika kuazimia kuyatimiliza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mtapewa mtihani, tena mtapewa mtihani, enyi Waumini, katika mali yenu kwa kutakiwa mtoe matumizi ya wajibu na yanayopendekezwa na kwa mikasa inayoyakumba. Pia mtapewa mtihani katika nafsi zenu kwa kutakiwa mtekeleze ya wajibu ya kumtii Allah Mtukufu na kwa misiba inayowafikia ya majaraha au mauaji na kuwakosa vipenzi vyenu. Hilo litaendelea mpaka apambanuke mwenye imani ya kweli na mwenginewe. Na mtasikia, tena mtasikia, kutoka kwa Mayahudi, Wanaswara na washirikina maneno yatakayoudhi masikizi yenu katika matamshi ya ushirikina na kuitukana dini yenu. Na iwapo mtasubiri, enyi Waumini, juu ya hayo yote na mkamcha Allah Mtukufu kwa kujilazimisha kumtii Yeye na kujiepusha na kumuasi, hakika hilo ni miongoni mwa mambo ambayo yanakusudiwa kidhati na kushindaniwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net