Aal-i-Imraan 3:189
آل عمرانوَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Na ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Ufalme wa Mbingu na Ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [189]
[189] Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mwenye mamlaka ya kila jambo la Mbinguni na duniani. Naye ni Muweza wa kila kitu. Atawashika wenye dhambi kwa dhambi zao, na atawalipa thawabu watendao mema kwa wema wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni wa Allah Mtukufu, Peke Yake, ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo humo. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net