Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 162

Aal-i-Imraan 3:162

آل عمران

أَفَمَنِ ٱتَّبَعَ رِضْوَٰنَ ٱللَّهِ كَمَنۢ بَآءَ بِسَخَطٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأْوَىٰهُ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Je, aliyeyafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliyerudi na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makazi yake yakawa Jahannamu? Napo ndipo pahali pabaya mno pa kurejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliye stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake yakawa Jahannamu? Napo ni mahala pabaya pa kurejea. [162]

[162] Hawawezi kuwa sawa, anaye piga mbio kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa vitendo na ut'iifu, na yule anaye stahiki ghadhabu kuu ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya uasi wake. Na mwenye kuasi ataishia Jahannamu, na kuovu kulioje huko!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yule ambaye lengo lake ni radhi za Allah Mtukufu, halingani na yule ambaye amebobea kwenye maasia na kumkasirisha Mola wake na akastahiki kwa hilo makazi ya Jahanamu ambayo mwisho mbaya wa mtu kuishilia ni hapo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net