Aal-i-Imraan 3:163
آل عمرانهُمْ دَرَجَـٰتٌ عِندَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِمَا يَعْمَلُونَ
Hao wana vyeo mbalimbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao wana vyeo mbali mbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo. [163]
[163] Makundi mawili hayo hayawi sawa, bali yametafautiana mbele ya Mwenyezi Mungu kwa daraja mbali mbali. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zao na daraja zao, na atawalipa kwa mujibu wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wa Peponi wenye kufuata yenye kumridhisha Allah Mtukufu wanatafautiana daraja. Na watu wa Motoni wanaofuata yenye kumkasirisha Allah Mtukufu wanatafautiana. Wao hawalingani. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuziona amali zao, hakifichiki chochote Kwake katika matendo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net