Aal-i-Imraan 3:161
آل عمرانوَمَا كَانَ لِنَبِىٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Na haikuwa kwa Nabii yeyote kufanya hiyana. Na atakayefanya hiyana, atakuja Siku ya Kiyama na kile alichofanyia hiyana, kisha kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa. [161]
[161] Haisihi kuwa Nabii yeyote kukhuni katika ngawira kama walivyo eneza kwa uzushi wanaafiki waongo. Kwani khiyana ni kinyume na Unabii. Basi isikupitikieni dhana hiyo. Na mwenye kukhuni atakuja Siku ya Kiyama na mzigo wa dhambi wa khiyana yake, tena kila nafsi italipwa ilicho tenda, kwa ukamilifu. Na wala hawatadhulumiwa kwa kupunguzwa thawabu zao wala kuzidishiwa adhabu yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haiwi kwa Mtume kuwafanyia hiana maswahaba wake kwa kutwaa kitu katika ngawira ambayo Allah Mtukufu Hakumtengea. Na yoyote mwenye kulifanya hilo, miongoni mwenu, atakuja Siku ya Kiyama akiwa amekibeba kile alichokitwaa, ili afedheheshwe nacho mbele ya kila mtu katika kisimamo kinachojumuisha watu wote. Kisha itapewa kila nafsi malipo kamili ya ilichokichuma pasi na kupunguzwa wala kufanyiwa dhuluma.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net