Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 160

Aal-i-Imraan 3:160

آل عمران

إِن يَنصُرْكُمُ ٱللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا ٱلَّذِى يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعْدِهِۦ ۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Maana

Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna wa kukushindeni. Na akikutupeni, basi ni nani huyo baada yake atakayekunusuruni? Na kwa Mwenyezi Mungu tu, basi na wategemee Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. [160]

[160] Mwenyezi Mungu akikuungeni mkono kwa nusura yake, kama ilivyo tokea siku ya Badri, hatokushindeni yeyote. Na akikuacheni mkono kwa kuwa nyinyi hamkuchukua khatua zifaazo za ushindi, kama yaliyo pita siku ya Uhud, basi hamtakuwa na wa kukunusuruni mwenginewe. Na ni juu ya Mwenyezi Mungu peke yake ndio yawapasa Waumini wategemeze mambo yao yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Iwapo Allah Mtukufu Atawapa msaada na nusura Yake, hapana yoyote awezaye kuwashinda. Na iwapo Atawaacha kuwasaidia na kuwanusuru, basi ni nani awezaye kuwanusuru nyinyi baada ya Yeye kuacha kuwanusuru? Na kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, nawajitegemeze Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net