Aal-i-Imraan 3:159
آل عمرانفَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلْقَلْبِ لَٱنفَضُّوا۟ مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَٱعْفُ عَنْهُمْ وَٱسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِى ٱلْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَوَكِّلِينَ
Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe, na waombee kufutiwa dhambi, na shauriana nao katika mambo. Na ukishakata shauri, basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea. [159]
[159] Ilikuwa ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwako wewe (Muhammad) na kwao (Waumini) kwa kuwa wewe umekuwa laini kwao wala hukuwatolea neno la ukali kwa kukosea kwao. Na lau kuwa wewe ungeli kuwa unawachukulia kwa ukavu, na moyo mgumu wangeli kukimbia. Basi nawe yapuuze makosa yao, na waombee msamaha, na ushauriane nao katika mambo ili upate maoni yao katika mambo ambayo siyo ulio teremshiwa ufunuo, Wahyi. Ukisha funga azimio lako juu ya jambo baada ya kushauriana, basi endelea nalo na huku ukimtegemea Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu humpenda anaye mwakilisha mambo yake Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa ajili ya rehema za Allah Mtukufu kwako na maswhaba wako, ewe Nabii, Allah Mtukufu Alikuneemesha ukawa laini kwao. Na lau ungalikuwa na tabia mbaya, mwenye moyo mgumu, maswahaba wako wangalijitenga na kuwa mbali na wewe. Kwa hivyo, usiwe na hasira nao kwa yaliyotokea kwao katika vita vya Uḥud. Basi muombe Allah Mtukufu, ewe Nabii, Awasamehe na uwashauri katika mambo yanayohitajia ushauri. Na utakapoazimia kufanya jambo kati ya mambo yoyote, baada ya kushauri, litekeleze hali ya kumtegemea Allah Mtukufu Peke Yake. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda wenye kujitegemeza Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net