Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 158

Aal-i-Imraan 3:158

آل عمران

وَلَئِن مُّتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى ٱللَّهِ تُحْشَرُونَ

Maana

Na mkifa au mkiuliwa, basi ni kwa Mwenyezi Mungu ndiko mtakakokusanywa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkifa au mkiuliwa ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mtakusanywa. [158]

[158] Na lau mtakufa au mtauliwa katika Jihadi hazitopotea bure a'mali zenu, kwani mtakusanywa kwa Mwenyezi Mungu akulipeni kwa Jihadi yenu na ikhlasi yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo ajali zenu zitakoma katika haya maisha ya dunia na mkafa juu ya matandiko yenu au mkauawa katika uwanja wa mapigano, ni kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, Mtakusanywa; na huko Atawalipa kwa matendo yenu mliyoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net