Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 157

Aal-i-Imraan 3:157

آل عمران

وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

Maana

Na mkiuliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au mkifa, hakika kufutiwa dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na rehema ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pindi mkiuliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au mkifa, hakika maghfira na rehema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote wanayo yakusanya. [157]

[157] Na mkiuwawa katika Jihadi au mkafa wakati huo, basi hayo hakika ni kupata maghfira ya Mwenyezi Mungu kufutiwa dhambi zenu, na kupata rehema itokayo kwake. Hayo ni bora kuliko starehe za dunia ambazo mnge zikusanya lau mngeli bakia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo mtauawa, enyi Waumini, katika hali ya kupigana katika njia ya Allah Mtukufu au mkafa vitani, Allah Mtukufu Atawasamehe madhambi yenu na Atawarehemu rehema itokayo Kwake. Hapo mtafaulu kwa kuyapata mabustani ya Peponi yenye starehe nyingi. Hayo ni bora kuliko dunia na wanavyovikusanya wapenda dunia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net