Aal-i-Imraan 3:156
آل عمرانيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَقَالُوا۟ لِإِخْوَٰنِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ أَوْ كَانُوا۟ غُزًّى لَّوْ كَانُوا۟ عِندَنَا مَا مَاتُوا۟ وَمَا قُتِلُوا۟ لِيَجْعَلَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِى قُلُوبِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakawaambia ndugu zao wanaposafiri katika nchi au wanapokuwa vitani: 'Lau wangelikuwa nasi, wasingelikufa na wasingeliuwawa.' Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto makubwa katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona vyema mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru na wakawasema ndugu zao walipo safiri katika nchi au walipo kuwa vitani: Wangeli kuwa kwetu wasingeli kufa na wasingeli uwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo. [156]
[156] Enyi mlio amini! Msiwe kama walio kufuru wakasema, kwa mintarafu ya wenzao wanapo ondoka kwenda safarini kutafuta maisha wakafa, au wakenda vitani wakauwawa: Lau wangeli bakia nasi hapa wasingeli kufa, na wasingeli uwawa. Mwenyezi Mungu amejaalia kauli yao hiyo na dhana yao iwe ni majuto ya nyoyoni mwao. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha, na kudra ya kila kitu imo mikononi mwake. Yeye anayajua yote myatendayo, ya kheri na shari. Na Yeye ndiye wa kukulipeni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msijifananishe na makafiri ambao hawamuamini Mola wao. Kwani wao huwaambia ndugu zao, miongoni mwa makafiri, wanapotoka kwenda kutafuta maisha yao katika ardhi au wanapokuwa pamoja na wapiganaji, wakafa au wakauawa, «Lau kama hawa hawangetoka wala hawangepigana na wakabakia pamoja na sisi, hawangekufa wala hawangeuawa.» Neno hili linawaongezea machungu, maudhiko na majuto yanayobakia katika nyoyo zao. Ama Waumini, wao wanajua kwamba hili limetokana na kadara ya Allah Mtukufu, ndipo Allah Mtukufu Huziongoza nyoyo zao na Huwasahilishia misiba. Na Allah Mtukufu Anambakisha hai yule Aliyemkadiria kuishi, hata kama ni msafiri au ni mpiganaji. Na Anamfisha yule ambaye muda wake wa kuishi umekoma, hata kama ni mkazi wa mji. Na Allah Mtukufu kwa kila mlifanyalo ni Mwenye kuliona, na Atawalipa kwalo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net