Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 155

Aal-i-Imraan 3:155

آل عمران

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوْا۟ مِنكُمْ يَوْمَ ٱلْتَقَى ٱلْجَمْعَانِ إِنَّمَا ٱسْتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا۟ ۖ وَلَقَدْ عَفَا ٱللَّهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ

Maana

Hakika, wale waliogeuka wakakimbia miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili, hakika Shetani tu ndiye aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya. Na Mwenyezi Mungu amekwishawasamehe. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio rudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana majeshi mawili, Shet'ani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyo yafanya; na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole. [155]

[155] Enyi jamaa wa Kiislamu! Wale miongoni mwenu walio acha kusimama imara pale pahali pao walipo wekwa wasimame hakika ni Shetani ndiye aliye wavuta kwenye utelezi na kukosea kwa sababu ya makosa yao kumkhaalifu Mtume. Lakini Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe, kwani Yeye ni mwingi wa maghfira, na mwingi wa upole.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliokimbia kati yenu, enyi Maswahaba wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwenye vita siku waliokutana Waumimini na washirikina katika vita vya Uḥud, ni Shetani ndiye aliyewatosa kwenye dhambi hili kutokana na baadhi ya madhambi waliyoyafanya. Kwa kweli Allah Mtukufu Amewasamehe na hakuwaadhibu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa Msamaha kwa wenye madhambi wanaotubia, ni Mpole Asiyekuwa na haraka ya kuwatesa wenye kumuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net