Aal-i-Imraan 3:133
آل عمرانوَسَارِعُوٓا۟ إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا ٱلسَّمَـٰوَٰتُ وَٱلْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
Na kimbilieni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na Bustani ambayo upana wake ni mbingu na ardhi. Iliandaliwa kwa ajili ya wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni Mbingu na Ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu, [133]
[133] Na kuweni wa mbele katika kutenda mema ili mpate kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki mambo yenu yote, maghfira makubwa ya kufutiwa dhambi zenu, na Pepo yenye wasaa, na upana wake ni kama upana wa Mbingu zote na Ardhi. Hayo wametengenezewa wale wanao mcha Mwenyezi Mungu na wakaiogopa adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kimbilieni, kwa kumtii kwenu Allah Mtukufu na Mtume wake, ili kupata msamaha mkubwa utokao kwa Mola wenu na mpate Pepo kunjufu, upana wake ni sawa na mbingu na ardhi, Ameiandaa Mweyezi Mungu kwa wachamungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net