Aal-i-Imraan 3:132
آل عمرانوَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa. [132]
[132] Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume katika kila wanacho amrisha na kila wanacho kikataza ili mpate kurehemeka duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mtiini Allah Mtukufu, enyi waumini, katika yale Aliyowaamrisha kwayo ya twaa na yale Aliyowakataza nayo ya kula riba na mengineyo. Na mtiini Mtume ili mpate kurehemewa na msiadhibiwe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net