Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 134

Aal-i-Imraan 3:134

آل عمران

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِى ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلْكَـٰظِمِينَ ٱلْغَيْظَ وَٱلْعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Wale ambao hutoa wanapokuwa katika nyakati nzuri na wanapokuwa katika dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na ni wasamehevu kwa watu. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema; [134]

[134] Hao wachamngu ndio wale wanao toa mali yao kwa kumridhi Mwenyezi Mungu wanapo kuwa na neema na wasaa, na pia wanapo kuwa na shida na dhiki na uzito, na wanazuia ghadhabu zao wanapo kasirishwa wasiwaadhibu wale wanao wakosa, bali wanawasamehe walio watendea mabaya. Hao kwa haya huhisabiwa kuwa ndio watenda mema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu huwalipa mema hao watenda mema na huwa radhi nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao wanatoa mali yao katika hali ya wepesi na uzito, na wanaozuia hasira zilizo ndani ya nafsi zao kwa kusubiri, na wanaowasamehe waliowadhulumu wanapokuwa na uwezo. Huu ndio wema ambao Allah Mtukufu Anawapenda wenye kuwa nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net