Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 110

Aal-i-Imraan 3:110

آل عمران

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ ۗ وَلَوْ ءَامَنَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ

Maana

Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu waliamini, ingelikuwa bora kwao. Miongoni mwao wako Waumini, lakini wengi wao ni wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu. [110]

[110] Nyinyi Umma wa Muhammad ni bora ya umati alio umba Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya watu, maadamu mtaamrisha ut'iifu na mtakataza maasi, na mtakuwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Imani safi na ya kweli. Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeli kuwa ni wakweli katika imani yao kama nyinyi, basi ingeli kuwa ni bora kwao kuliko walivyo. Walakini baadhi yao ni Waumini, na wengi wao wameikiuka mipaka ya Imani na yanayo pasa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nyinyi, enyi umma wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni bora wa ummah na ni watu wenye manufaa zaidi kwa watu, mnaamrisha mema, nayo ni yale yanayofahamika uzuri wake kisheria na kiakili, na mnakataza maovu, nayo ni yale yanayoeleweka ubaya wake kisheria na kiakili, na mnamuamini Allah Mtukufu kikweli kweli imani inayotiliwa nguvu na vitendo. Na lau kama Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wangalimuamini Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na yale aliyowajia nayo kutoka kwa Allah Mtukufu kama mlivyoamini nyinyi, lingekuwa hilo ni bora kwao duniani na Akhera. Katika hao wako Waumini waukubalio ujumbe wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, wanaoufuata kivitendo ujumbe huo, nao ni wachache. Na wengi wao ni watokaji nje ya dini ya Allah Mtukufu na twaa Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net