Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 111

Aal-i-Imraan 3:111

آل عمران

لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّآ أَذًى ۖ وَإِن يُقَـٰتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ ٱلْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ

Maana

Maadui hawatawadhuru isipokuwa kwa maudhi tu. Na wakipigana nanyi, watawapa migongo, kisha hawatanusuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [111]

[111] Hao wapotovu hawawezi kukudhuruni nyinyi kama walivyo kuandalieni, wala hawakuathirini. Ijapo kuwa mtapata maudhi kwao, lakini athari yake haiselelei. Na hata wakipigana nanyi wataingia kiwewe wakimbie wasipambane nanyi, na hapo mwishoe hawatopata ushindi juu yenu maadamu nyinyi mtashikamana na kuamrisha mema na kukataza maovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawatawadhuru nyinyi hawa watu waovu, miongoni mwa watu waliopewa Vitabu, isipokuwa kile kitakachoyaudhi masikizi yenu cha matamshi ya ushirikina na ukafiri na mengineyo. Na wakiwapiga vita, watashindwa na watakimbia hali ya kuwapa mgongo, kisha hawatapata ushindi juu yenu kwa hali yoyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net